Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Sera na Mipango

IDARA YA SERA NA MIPANGO

JUKUMU KUU

Kutoa utaalam na huduma katika sera, mipango, maandalizi ya bajeti; na utafiti na uvumbuzi.


Idara ina Sehemu Mbili (2):

(i) Sehemu ya Sera, Utafiti na Ubunifu; na 
(ii) Sehemu ya Mipango na Bajeti.

Idara inaongozwa na; 

          Bi. Joyce Jonathan Momburi

    Mkurugenzi wa Sera na Mipango (DPP)
Email: 
joyce.momburi@mawasiliano.go.tz

WASIFU 

Joyce Jonathan Momburi ni Mkurugenzi katika Idara ya Sera na Mipango, aliyebobea kwenye Sera na Mipango. Kiongozi mwenye uwezo wa kufanya kazi nyingi katika kuratibu, uandaaji wa Sera na Sheria za Sekta pamoja na kupitia upya zilizopo. Amefanikiwa kuratibu shughuli za Sekta, Ufuatiliaji na Tathmini ya programu/miradi mbalimbali, Kutayarisha Sera, miongozo yake;

Amezaliwa na kukulia Mkoani Kilimanjaro, Wilaya ya Siha. Joyce alitunukiwa Diploma ya Uchumi katika Maendeleo, Chuo Kikuu cha Bradford, Uingereza; Diploma ya Juu ya Mipango ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, Tanzania na Baadae kutunukiwa Shahada ya Uzamili wa Sanaa katika Mafunzo ya Maendeleo ya Kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Bradford, Uingereza.

Joyce, alifanikiwa kufanya kazi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kama Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathmini, Mkurugenzi Msaidizi (Sera); Wizara ya Fedha, Mipango kama Mchumi na Mchumi Mkuu mtawalia na Afisa Mipango na Udhibiti - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Dar es Salaam.

Joyce anabaki kuwa mfano wa kuigwa katika kuhakikisha kuwa Malengo, Mikakati ya Wizara iliyoainishwa kwenye Mipango Mkakati yanafikiwa kwa manufaa ya Sekta na Nchi kwa ujumla.


MAJUKUMU YA IDARA YA SERA NA MIPANGO

(1) Sehemu ya Sera, Utafiti na Ubunifu;

(i) Kuratibu maendeleo na utekelezaji wa sera za Wizara;

(ii) Kuratibu Mapitio ya sera za Wizara;

(iii) Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa sera za Wizara;

(iv) Kupitia na kushauri juu ya nyaraka za sera zilizotayarishwa na Wizara nyingine;

(v) Kuandaa miongozo kuhusu masuala ya utafiti na ubunifu.

(vi) Kuratibu masuala ya tafiti na bunifu kwa lengo la kufanya maamuzi yenye tija:

(vii) Kuratibu usimamizi wa masuala ya bunifu katika Wizara;

(viii) Kushirikiana na taasisi za utafiti wa kitaifa na kimataifa na vituo vya data kwa lengo la kukusanya na kubadilishana taarifa za tafiti na bunifu.

(ix) Kuyatambua maeneo ya tafiti na vipaumbele kwa Wizara; na

(x) Kuandaa mikakati ya utekelezaji na usambazaji wa matokeo ya tafiti.


(2) Sehemu ya Mipango na Bajeti.

 

Sehemu hii itatekeleza shughuli zifuatazo:

(i) Kuratibu maandalizi ya mpango mkakati wa Wizara, mipango ya utekelezaji na bajeti;

(ii) Kuratibu maandalizi ya Hotuba ya Bajeti kwa Wizara;

(iii) Kupitia mipango na programu zilizotekelezwa katika Wizara;

(iv) Kuratibu maandalizi ya Ripoti za Utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa kila robo mwaka;

(v) Kuandaa taarifa za utekelezaji wa Ilani, maagizo ya Serikali, na masuala ya Bunge;

(vi) Kuandaa mikakati ya kukusanya rasilimali kwa Wizara;

(vii) Kuandaa nyaraka za miradi na programu kwa ajili ya upatikanaji wa fedha;

(viii) Kutoa mwongozo wa kitaalamu na usaidizi wa katika mchakato wa mipango kazi na bajeti ndani ya Wizara;

(ix) Kufanya ufuatiliaji wa utoaji wa huduma za Wizara.

(x) Kuratibu ufanyikaji wa Tathmini ya Wizara (Tathmini ya Taasisi);

(xi)Kuratibu maandalizi, utekelezaji na usimamizi wa vihatarishi kwa Wizara; na

(xii) Kuratibu maendeleo ya programu na miradi ya Wizara.