Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Maelezo Kuhusu Wizara

HISTORIA                                                  

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ilianzishwa tarehe 12 Septemba, 2021 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wizara iliunganisha majukumu yaliyokuwa yakitekelezwa na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari hapo awali na Idara ya Habari ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Wizara inalenga kutunga na kusimamia utekelezaji wa sera za teknolojia ya habari, mawasiliano, habari na huduma za Posta. Inakusudiwa kuendesha ajenda ya mabadiliko ya kidijitali nchini Tanzania katika awamu ya nne ya mapinduzi ya viwanda duniani pamoja na kukuza upashanaji taarifa wenye tija.

MAJUKUMU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliunda Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari tarehe 12 Septemba, 2021 ambayo ina jukumu la kutunga na kufuatilia utekelezaji wa Sera za Habari, Teknolojia ya Habari, Mawasiliano na Posta. Wizara pia inawajibika katika kusimamia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano; Uboreshaji wa Utendaji na Maendeleo ya Rasilimali Watu; Msemaji Mkuu wa Serikali; Idara za ziada za Wizara, Mashirika ya Umma; Wakala na Miradi iliyo chini ya Wizara hii.

MAADILI YETU

Uadilifu: Tunawatendea wateja wetu na wadau wengine kwa haki na kwa adabu. Tunazingatia maadili wakati wa kutekeleza majukumu yetu na kudumisha usiri.

Uwazi: Tunasambaza taarifa muhimu kuhusu huduma na bidhaa zetu kwa umma.

Kazi ya pamoja: Tunatumia utaalamu mbalimbali katika kufikia malengo yetu.

Taaluma/Uweledi: Tunatumia ustadi wa hali ya juu na umahiri katika kutekeleza majukumu yetu.

Ubunifu: Tunatengeneza mbinu na mawazo mapya ambayo husababisha matokeo chanya katika sekta hii.

Uwajibikaji: Tunawajibika kwa vitendo na maamuzi tunayofanya wakati wa kutekeleza majukumu yetu.