Miradi Iliyo Kamilika
ORODHA YA MIRADI ILIYOKAMILIKA |
||||||
Na. |
JINA LA MRADI |
MUDA WA UTEKELEZAJI WA MRADI |
TAREHE YA KUANZA KWA MRADI |
TAREHE YA KUKAMILIKA KWA MRADI |
MAENEO YA MRADI/ WAFAIDIKA NA MRADI
|
MFADHILI |
1. |
Mradi wa Ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano Awamu ya I. |
Miezi 18 |
2009 |
2010 |
Katika mradi huu wa Ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano Awamu ya I jumla ya kilomita 2,280 zilijengwa. Aidha, katika Awamu hii Mkongo wa Taifa uliunganishwa pia na Mikongo ya Baharini ya SEACOM na EASSy. |
Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kupitia mkopo wenye Masharti nafuu kutoka Benki ya Exim ya China |
2. |
Mradi wa Ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano Awamu ya II. |
Miezi 18 |
2010 |
2012 |
Katika mradi huu wa Ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano Awamu ya II jumla ya kilomita 3,168 zilijengwa. |
|
3. |
Mradi wa Ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano Awamu ya III. |
Miezi 18 |
2014 |
2016 |
Katika Ujenzi wa Mkongo wa Taifa Awamu ya III jumla ya Kilomita 100 zilijengwa Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya na Pemba. Awamu hii ilijumuisha ujenzi wa Kituo cha Taifa cha Data (National Internet Data Centre) Dar es Salaam, ufungaji wa mitambo kwa ajili ya mtandao wa miundombinu ya itifaki [Internet Protocol-Multilayer Label Switching (IP-MPLS) Network], Upanuzi wa Mkongo na kuunganisha Zanzibar kwenye Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano. Aidha, hadi sasa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano umeunganisha Makao Makuu ya mikoa 25 ya Tanzania Bara ambapo katika Mikoa hiyo Mkongo wa Taifa umefika kwenye Wilaya 42 kati 139 na una urefu wa Kilomita 7,910. |
|
4. |
Mradi wa kuunganisha Ofisi za Halmashauri kwenye Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano. |
Miezi 10 |
Juni 2018 |
Aprili 2019 |
Mradi huu umehusisha kuunganisha kwenye mawasiliano Halmashauri 10 zifuatazo; Katesh, Uvinza, Wanging’ombe, Urambo, Kaliua, Mbulu, Monduli, Sikonge, Simanjiro na Kiteto. |
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania |
5. |
Mradi wa kuunganisha Ofisi mbalimbali za Serikali pamoja na Halmashauri zipatazo kwenye Mkongo wa Taifa wa mawasiliano |
Miezi 12 |
Agosti 2019 |
Agosti 2020 |
Mradi huu umehusisha kuunganisha kwenye mawasiliano jumla ya Ofisi 18 za Serikali pamoja na Halmashauri zilizopo katika mikoa ya Mwanza, Dodoma, Kagera, Mbeya, Arusha, Mtwara, Lindi, Geita, Shinyanga, Tanga na Pwani. Ofisi zilizounganishwa ni; Igoma Kituo cha Afya, Misungwi Kituo cha Afya, Kisesa Kituo cha Afya, Maktaba ya Dodoma, Kituo cha Afya Makole, Hospitali ya Mirembe, Halmashauri ya Kondoa, Halmashauri ya Ileje, Ngarenaro Kituo cha Afya, Kaloleni Kituo cha Afya, Halmashauri ya Mtwara, Halmashauri ya Lindi, Nyangao Hospitali, Halmashauri ya Geita, Halmashauri ya Kishapu, Maramba Kituo cha Afya-Mkinga, Ngamiani Kituo cha Afya na Halmashauri ya Mafia. |
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
|
6. |
Mradi wa kuunganisha Ofisi mbalimbali za Serikali na Halmashauri kwenye Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano. |
Miezi 15 |
Mei 2019 |
Agosti 2020 |
Mradi huu ulihusisha kuunganisha ofisi 23 za Serikali pamoja na Halmashauri zilizopo kwenye mikoa ya Kilimanjaro, Geita, Arusha, Morogoro, Katavi, Rukwa, Kigoma, Mbeya, Mwanza na Geita, kuunganishwa kwa mawasiliano kwa njia ya mkongo. Na pia mradi huu ulihusisha ukarabati wa Njia ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ya Arusha-Namanga. Ofisi kutokana na mradi huu ni zifuatazo; Posta Siha, Siha Hospitali ya Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya-Siha, Mkuu wa Wilaya-Siha, Mkurugenzi Mtendaji-Bukombe, Bukombe Hospitali, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya-Ngorongoro, Mkuu wa Wilaya-Ngorongoro, Mahakama-Ngorongoro, Magereza-Ngorongoro, Polisi-Ngorongoro, Ngorongoro Hospitali, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya-Mvuha, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya-Nsimbo, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya-Mlele, Ofisi ya Rais-Mlele, Mkurugenzi Mtendaji Wilaya-Kalambo, Mkurugenzi Mtendaji Wilaya-Buhigwe, Buhigwe Hospitali, ITETE DDH, Mkuu wa Wilaya-Busekelo, Mkurugenzi Mtendaji Wilaya-Buchosa, na Buchosa Hospitali. |
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
|
7. |
Mradi wa kuwezesha Miundombinu ya Mawasiliano ya Kikanda Tanzania- Tanzania Communications Infrastructure and eGovernment Project (Regional Communications Infrastructure Program – RCIP Tanzania Project)
|
Miezi 84
|
Januari 2010
|
Desemba 2017 |
Utekelezaji wa mradi huu umekuwa na matokeo chanya na kufikia malengo yaliyokusudiwa. Baadhi ya Matokeo hayo ni kama ifuatavyo;
umekamilika na unaendelea kutumika na kuweza kusaidia upatikanaji wa haraka wa kumbukumbu na nyaraka mbalimbali za Serikali na pia kuongeza ufanisi wa uhifadhi na upatikanaji (kwa njia ya kielectroniki) wa kumbukumbu hizo kwa taasisi za serikali, watafiti na wananchi kwa ujumla;
|
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia mkopo kutoka Benki ya Dunia |