Habari
WIZARA YASHIRIKI KIKAO CHA MAKAMU WA RAIS NA USAID
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) wakati akiwasili katika Hospitali ya Mount Meru katika ziara yake na Balozi Samantha Power juu ya Mfumo wa Kurahisisha Usafiri wa Dharura kwa Mama Wajawazito na Watoto Wachanga wa m-mama katika jiji la Arusha, Tarehe 22 Juni, 2023.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) ameshiriki kikao cha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip na Mkuu wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) , Balozi Samantha Power, kikao hicho kimefanyika katika Hoteli ya Gran Melia, jijini Arusha, leo Juni 22, 2023.
Miongoni mwa walioshiriki kikao hicho ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Selestine Gervas Kakele.