Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

WIZARA YAKUTANA NA WADAU WA HABARI KUTOA MAONI YA RASIMU YA SERA YA TAIFA


Na Chedaiwe Msuya, WHMTH, Da es Salaaam.

Tarehe 28 Septemba,2023 Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imekutana na Wadau wa Habari kupitia kwa pamoja na kutoa maoni kuhusu rasimu ya sera ya Taifa ya TEHAMA.

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari inajukumu la kutunga na kusimamia utekelezaji wa sera ya TEHAMA nchini.

Kwa jukumu hilo Wizara iliweza kuanda mkutano huo na Wadau waweze kutoa maoni namna ya sera hiyo itakavyoleta mabadiliko chanya kwa Taifa.


Sera hii itaweza kujenga na kulinda usalama wa Wadau na watu wengine katika jamii

Kikao hicho kimehudhiriwa na viongozi mbalimbali wa Wizara pamoja na watumishi wa Wizara na Wadau wa Habari.