Habari
WIZARA YAFANYA MAPITIO YA NAMNA YA UTEKELEZAJI WA MFUMO WA PEPMIS

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari pamoja na taasisi zake za Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imefanya mapitio ya namna ya utekelezaji wa mfumo wa Usimamizi na Utendaji kazi katika utumishi wa Umma (PEPMIS) chini ya Usimamizi wa wataalamu kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Mapitio ya utekelezaji wa Mfumo huo yanafanyika leo Mei 22 jijini Dodoma katika ngazi ya Wakuu wa Idara, Sehemu, Kitengo na ngazi ya maafisa.