Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

WHMTH YAJADILI MASHIRIKIANO NA TAASISI YA DCO YA SAUDI ARABIA


Na Mwandishi Wetu, Saudi Arabia

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Mohammed Khamis Abdulla pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi (Zanzibar) Bi. Khadija Khamis Rajab wamekutana na kufanya mkutano na Mtendaji Mkuu pamoja na viongozi wengine wa Taasisi ya Digital Coorporation Organisation (DCO) katika makao makuu ya taasisi hiyo yaliyopo Riyadhi, Saudi Arabia kwa lengo la kujadili Ushirikiano na taasisi hiyo.  

Taasisi hiyo (DCO) yenye nchi wanachama 15 iliundwa kwa lengo la kuinua kiwango cha ushirikiano  na kubadilishana uzoefu wa kisera, mifumo, mikakati na mbinu kwa nchi wanachama ya matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano  katika kuchochea ukuaji wa uchimi na Maendeleo ya jamii. 

Kikao hicho kilichofanyila tarehe 3 Oktoba 2023 na kilihudhuriwa na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Dr. Mohamed Juma Abdallah.

Pichani matukio mbalimbali ya ujumbe wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi (Zanzibar) katika kikao hicho.