Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

WAZIRI NAPE AZINDUA INTANETI YA WAZI (FREE-WIFI) SABASABA


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye amezindua huduma ya Intaneti ya Wazi (Free-Wifi) katika maeneo 17 ndani ya Viwanja vya Maonesho ya Sabasaba, leo tarehe 8 Julai, 2023, ikiwa ni siku ya TEHAMA katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (Sabasaba).

Huduma hiyo ya Intaneti ya wazi imewezeshwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa kushirikiana na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

#SabaSaba #TzyaKidijitali #KaziIendelee

Matukio mbalimbali katika picha wakati Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) akizindua huduma ya mtandao wa intaneti ya wazi (free wiFi) inayotolewa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa kushirikiana na TTCL katika maeneo 17 ya  viwanja vya Maonesho ya Sabasaba.Waziri Nape aliambatana na   Naibu wake Mhe. Mhandisi Kundo Mathew, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Selestine Gervas Kakele na baadhi ya Wakurugenzi, Wakuu wa Taasisi na wadau wa Wizara hiyo, leo Julai 8,2023,  jijini Dar es Salaam.