Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

WAZIRI NAPE AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KATIBU MKUU WA UPU NCHINI SAUDI ARABIA


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Nape Moses Nnauye leo amefanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Duniani (UPU) Bwana Masahiko Metoki. 

Mazungumzo hayo yaliwahusisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bwana Mohammed Abdulla, Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) Bwana Maharage Chande na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Balozi Ali Jabir Mwadini. 

Pichani ni matukio mbalimbali wakati ujumbe wa Mhe. Nape Nnauye ulipokuwa katika mazungunzo na Katibu huyo Mkuu wa UPU.