Habari
WAZIRI NAPE AFANYA UZINDUZI WA KITUO CHA TBC KATAVI
Na Chedaiwe Msuya - WHMTH
Shirika la utangazaji Tanzania (TBC) limezindua kituo kipya cha matangazo cha TCB Taifa na TBC Fm katika mkoa wa katavi ikiwa ni malengo ya serikali kuhakikisha inawafikia wananchi wote kwa ajili ya kuhabarisha na kuelimisha kwa njia ya redio na televisheni.
Uzinduzi huo umefanywa na Waziri wa Habari, Mawasiliaono na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye (Mb) mapema hii leo ,ambapo amesema kuzinduliwa kwa kituo hicho ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa Taifa unaolenga kuongeza usikivu wa kituo hicho katika maeneo mbalimbali nchini.
Amesema Serikali inalojukumu la kufikisha huduma ya habari na mawasiliano kwa wananchi wote kutokana na mabadiliko ya teknolojia mitambo ya zamani ilishindwa kufanya kazi na hivyo kufanya kuwepo kwa ujenzi wa mitambo ya kisasa ili kuwezesha usikivu mzuri.
“Ujenzi wa miradi hii ya kuwezesha mawasiliano kuwafikia wananchi na utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi ambapo moja ya sera katika ilani yetu ni kuhakikisha tunapeleka usikivu wa TBC kwa wananchi wote.
“kadri tekinolojia inavyo badilika lazima na vifaa vibadilike zamani tulikuwa na teknolojia ya masafa ya kati lakini kwa sasa ime badilika kwa sasa kuna namna tunabidi tubadilike kulingana na teknolojia,”amesema
Sanjari na hayo Mhe. Nnauye amewataka wananchi kuendelea kutunza miundombinu hizo za mawasiliano na kutoa dhana ya kuwa mali hizo ni za serikali na kuzi haribu
Kwaupande wake Mbunge wa jimbo la katavi lililopo Halimashauri ya mlele mkoani Katavi Issack Kamwele ameiomba wizara hiyo kuwawezesha kupata huduma ya posta na miundombinu ya kuendesha huduma hiyo katika mkoa wa katavi.
Pia Mhe.kamwele ameliomba shirika la utangazaji Tanzania (TBC) kuwawezesha kutangaza mazao yanayopatikana katika mkoa huo ili kuwezesha upatikanaji wa masoko ya mazao yao
“Sisi huku tunamazao ya aina mbalimbali ikiwemo karanga, asali, tunakuomba sana ukatutangazie biashara ya asali na hapa nimeleta dumu moja ambalo nakukabidhi wewe ili ukaweze kututangazia biashara hii,”amesema.
Awali Mkurugenzi wa shirika la Utangazaji (TBC) Ayubu Rioba amesema mradi huo nimiongoni mwa miradi itakayo saidia usikivu wa matangazo ya shirika hilo nchini na matarajio ya shirika hilo mpaka miradi yote ikikamilika nikuongeza usikivu wa asilimia 92% nchini.
Pamoja na hayo amewashukuru wananchi wa mlele kwakuendelea kuliunga mkono shirika hilola la utangazaji na kuendelea kulionyesha ushirikiano.
“Katika ujenzi wa miradi hii kuna changamoto mbalimbali zinazo jitokeza lakini katika eneo hili sijaona changamoto yoyote na nimshukuru mbunge kwa kutuhakikishia huduma muhimu kuwepo maeneo haya,”amesema.
Naye Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya kudumu ya miundombinu , na Mbunge wa jimbo la Mpanda vijijini Selemani Kakoso amesema jitihada zilizofanywa na serikali ni kubwa na wananchi wanapaswa kudhamini jitihada hizo.
Amesema maelekezo ya kamati ya bunge yalikuwa nikupeleka usikivu katika maeneo yote na Mkoa wa katavi changamoto hiyo imekwisha kutatuliwa.
“Niomba sasa kupitia bajeti itakayotolewa mwaka huu muweze kujenga minara katika maeneo ya nkasi na wilaya ya uvinza ambapo asilimia kubwa wananchi wa maeneo hayo wanasikiliza redio za nje ya nchi na sio redio ya Taifa “, amesema.