Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

WATUMISHI WHMTH WAPATIWA VITENDEA KAZI


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Mohammed Khamis Abdulla amegawa vitendea kazi kwa watumishi wa Wizara hiyo kwa lengo la kuhakikisha utendaji wa Wizara hiyo unahamia kielektroniki kwa asilimia 100.

Akigawa vitendea kazi hivyo kwa Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo leo Mei 20, 2024 Bw. Abdulla amesema kuwa vitendea kazi hivyo ambavyo ni kompyuta za mezani (desktop), kompyuta mpakato (laptop) vishikwambi na printa vitawasaidia watumishi kukamilisha majukumu yao kwa wakati, itaongeza ufanisi na matumizi ya mifumo ya TEHAMA.