Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

WATENDAJI WA KATA NA MITAA NA WAKUSANYA TAARIFA WAAPISHWA KWAAJILI YA KUANZA RASMI UTEKELEZAJI WA MFUMO WA ANWANI ZA MAKAZI KATIKA MANISPAA YA UBUNGO


Na Simon Kibarabara

Leo Tarehe 21/06/2023 Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kupitia Wataalamu wa Mfumo wa Anwani za makazi imekamilisha zoezi la mafunzo kwa Watendaji wa Kata na Mitaa na wakusanya taarifa kuhusu zoezi la utekelezaji mfumo wa Anwani za Makazi katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwenye Ukumbi wa La Dariot uliopo jijini Dar es Salaam. 

Mafunzo hayo yametolewa kwa Watendaji wa Mitaa na Wakusanya Taarifa  zaidi ya 270 (mia mbili sabini) kwa ajili ya mitaa iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo yakiwa na lengo la kuboresha mfumo wa Anwani za Makazi kwa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.

Aidha, Watendaji wa Kata na Mitaa na  Wakusanya Taarifa waliweza kula Kiapo mbele ya Kamishna wa Viapo wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg. Erick Paul Bakilana na kusisitizwa kutunza siri na kufanya kazi kwa ufanisi na weledi.