Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

WATAALAMU SEKTA YA MAWASILIANO WATAKIWA KUTUMIA MAWAZO ENDELEVU NA KUTEKELEZA MAAZIMIO YA KIKAO KAZI CHA UCHAMBUZI WA FURSA ZA KIUCHUMI.


Na Chedaiwe Msuya

Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohammed Khamis Abdulla amewasisitiza wataalam wa sekta ya mawasiliano kutumia Mawazo Endelevu na kuyatekeleza yale waliyo azimia kwenye kikao kazi cha uchambuzi wa fursa za kiuchumi za sekta ya Mawasiliano Kitaifa na Kimataifa.
 
Naibu katibu Mkuu huyo ameyasema hayo tarehe 22 Juni, 2022 jijini Dodoma alipokuwa akifunga kikao hicho kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, amewataka wataalam wa TEHAMA kuwashirikisha Wataalamu wengine kutoka Taasisi mbalimbali kitaifa na Kimataifa ili wawe na mawazo ya pamoja katika kukuza fursa za kiuchumi za sekta ya mawasiliano Kitaifa nakimataifa.

"Angalieni sana sehemu za kwenda kujifunza, Mathalani unaenda nchi fulani unaenda kujifunza wale wanafanya nini, hili ndilo lengo la kikao hiki, tunahitaji kuona Mabadiliko katika sekta hii". Amezungumza Mohammed

Aidha, Naibu katibu Mkuu huyo amewataka wataalam hao kuchukua maoni ya wadau mbalimbali ili kupata uelewa mpana wa TEHAMA ambapo amewataka wataalam hao wa TEHAMA kuendeleza bunifu zao ili zilete tija na iwe mfano wa Mataifa Mengine kuja kuiga hapa nchini.

"Endelezeni Moto huu wala msichoke na mikakati hii mliyonayo ndio njia pekee ambayo itaitangaza sekta ya mawasiliano nchini kwa maendeleo ya Taifa"​ Amezungumza Mohammed

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala Bora Bi. Teddy Njau amesema kuwa wameainisha mikakati na njia za kutumia fursa zilizopo kwa Maendeleo ya Taifa ambapo amesema kuwa Maafisa TEHAMA watapatiwa ujuzi wa kutosha ili kuongeza wigo katika sekta ya Mawasiliano nchini.

Lengo la kikao kazi cha uchambuzi wa Fursa za kiuchumi za sekta ya Mawasiliano Kitaifa na Kimataifa ni kutafuta fursa kwenye masuala mbalimbali ya TEHAMA Kitaifa na Kimataifa ili kufikiwa kwa Malengo yaliyokusudiwa.