Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

TANZANIA NA JAMHURI YA AZERBAJAN KUSHIRIKIANA KATIKA TEHAMA


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa State Agency for Public Service and Innovations (SAPPS) iliyochini ya Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Azerbajan, Mhe. Ulvi Mehdiyev katika Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), leo Agosti 05, 2023 jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yamejikita zaidi katika mashirikiano baina ya Nchi hizo mbili hususani katika masuala ya sekta ya TEHAMA.

#TzyaKidijitali #KaziIendelee