Habari
SERIKALI KUWEKA WI-FI YA BURE VITUO VYA MWENDOKASI, MACHINGA COMPLEX, VYUO VIKUU
Na Juma Wange, WHMTH, Dar es Salaam
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) amesema Serikali kupitia Wizara hiyo itaweka Wi-Fi ya bure katika maeneo ya Machinga Complex, Vituo vya Mwendokasi na Vyuo Vikuu.
Waziri Nape ameyasema hayo mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhi Hassan Kuzindua Kituo cha Mkongo wa Baharini cha Airtel 2Afrika pamoja na Mtandao wenye kasi ya 5G wa Kampuni ya Mawasiliano ya Artel Tanzania iliyofanyika Mbezi Tanki Bovu, Dar es Salaam.