Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

SERIKALI KUTUNGA KANUNI ZITAKAZOLINDA MADHARA JUU YA TEKNOLOJIA YA AKILI MNEMBA (AI)


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) amethibitisha kwamba Serikali iko tayari kutunga kanuni zitakazolinda wananchi dhidi ya matumizi hasi yanayoweza kutokea kutokana na teknolojia ya Akili Mnemba (AI). 

Hatua hii inakuja baada ya swali la wasiwasi wa usalama lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalumu CCM kupitia Kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Mhe. Neema Lugangira, Bungeni jijini Dodoma leo Februari 09, 2024.