Habari
SERIKALI KULETA SULUHU YA MAWASILIANO TABORA VIJIJINI - NAIBU WAZIRI MHANDISI KUNDO
TABORA,
Naibu Waziri wa Habari, Mawsiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew (Mb) aahidi huduma bora za Mawasilino maeneo ya Tabora vijijini endapo tu wakazi wa maeneo hayo watashiriki kikamilifu katika zoezi la Mfumo wa Anwani za Makazi pamoja na Sensa ya watu na Makazi itakayofanyika Agosti, 2022.
Mheshimiwa Kundo alitoa kauli hiyo katika ziara yake ya kikazi ya ukaguzi wa upatikanaji huduma za Mawasiliano, mirada ya UCSAF katika maeneo ya pembezoni mwa Tabora mjini siku ya (Jumatano , Februari, 23 , 2022) wakati alipotembelea Kata ya Itetemia kitongoji cha Kipalapala na kukagua hate ulipofikia ujenzi wa mnara wa Mawasiliano kutoka kampuni ya Halotel na kumalizia ziara yake katika Vitongoji vya Ifucha, Kipalapala na Kakola ambapo alienda kutoa elimu juu ya mfumo huo pamoja na Sensa ya Watu na Makazi ya 2022 na kusikiliza maoni mbalimbali kutoka kwa wananchi wa vijiji hivyo kuhusu huduma za Mawasiliano.
Alisema kuwa Serikali ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imetenga kiasi cha fedha za Kitanzania Bilioni 28 ambacho kinaenda kutumika katika utekelezaji wa Mfumo wa Anwani za Makazi na kuwataka wananchi wa sehemu izokushiriki kikamilifu katika kutimiza zoezi hilo pamoja na kuhesabiwa ili iwe rahisi kwa Serikali kupeleka maendeleo katika maeneo yao kwa kujua idadi husika ya watu wanaoishi mahala hapo ikiwemo kuwapatia huduma bora za Mawasiliano kwa kuwekewa minara ya simu yenye ukubwa unao lingana na idadi watu hao.
“Mheshimiwa Rais kwa kulitambua hilo tayari amesha idhinisha kiasi cha Bilioni 28 za Kitanzania kwa ajili ya kutekeleza mradi huu wa Anwani za Makazi kwa kila Mtanzania hasa wananchi wa Kakola,Mheshimiwa Rais anafahamu mpo basi jitokezeni na mkahamasishe na wenzenu.”
“Watu wanaelewa nini miana ya kushiriki katika mazoezi haya mawili ya Anwani za Makazi na Postikodi pamoja na Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika mwezi Agosti, 2022, matokeo yake itakuwa ni rahisi kupata maendeleo kutokana na idadi ya watu wa eneo husikaIkiwemo huduma bora za Mawasiliano.”
“Mimi napenda sana nije Itetemia, napenda nije itetemia nikiwa nakuja kuzindua mradi huu sitaki nije itetemia kuwaahidi kitu kingine tena chochote, nataka kują Itetemia tukiwa tumewasha mnara huu na Wananchi mnafurahia uwepo wa Mawasiliano, hizo ndo salamu za Mhe. Rais hizo ndo salamu za Mhe. Waziri wangu na hizo ndo salamu za Serikali ya awamu ya sita.”
Pamoja na hayo, Mheshimiwa Kundo amesema mfumo huu wa Anwani za Makazi na Postikodi pamoja na Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika mnamo mwezi Agosti, 2022 vyote kwa pamoja vitatengeneza ajira kwa wananchi waishio maeneo ya vijiji vya Tabora mjini.