Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

SERIKALI HAINA MPANGO WA KUINGILIA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI- WAZIRI NAPE


Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) amesema Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuhakikisha watanzania wana kuwa huru kutoa maoni yao bila kuzuiwa. 

Ameyasema hayo Leo Februari 7, 2024 jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na taarifa ya Wasafi FM kuzuia mahojiano kati  ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo  (CHADEMA) na kituo cha redio hiyo kupitia kipindi chao cha Asubuhi.

Mhe. Nape amesisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita tangu iingie madarakani imeendelea kuimarisha demokrasia kwa kufungulia vyombo vya habari vilivyokuwa vimefungiwa na kufanya mapitio ya sera na sheria mbalimbali za sekta ya habari. 

"Nimekuja niseme serikali hatuna sababu ya kuingilia Uhuru wa vyombo vya habari, tumejitahidi tumetunga sheria, tunaimarisha taasisi zetu tunawahamasisha wasimamizi wa taasisi zetu kuhakikisha kuwa wanatoa Uhuru wa kutosha kwa wana habari ili watimize majukumu yao", amesema Mhe. Nape.