Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

RAIS SAMIA AAGIZA KUTUMIKA KWA NAMBA MOJA KWA KILA MTANZANIA


Na WHMTH, Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameiagiza Serikali kushirikiana na Taasisi mbalimbali kuondokana na mfumo wa kutumia namba nyingi uondolewe na kutaka mfumo utakaowawezesha kila Mtanzania kutumia namba moja ya utambulisho wake.

“Unakuta mtu ana namba moja ya NIDA lakini akienda Benki kuna taarifa nyingine nyingine, hospitali kuna taarifa nyingine, shule kuna taarifa nyingine. Sasa hii inasababisha ata usalama ndani ya Nchi unakuwa wa wasiwasi kidogo”. Amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Maagizo hayo yametolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Mkongo wa Baharini cha Airtel 2Afrika pamoja na Mtandao wenye kasi ya 5G wa Kampuni ya Mawasiliano ya Artel Tanzania iliyofanyika Mbezi Tanki Bovu, jijini Dar es Salaam.