Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

OFISI YA TUME YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI KUWA NA OFISI ZANZIBAR


Na Juma Wange, WHMTH, Zanzibar

Leo Septemba 08, 2023 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Ndugu Khadija Khamis Rajaab amekutana na kuzungumza na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiluano naTeknolojia ya Habari Bara, Selestine Gervas Kakele katika ofisi za Wizara hiyo, Zanzibar.

Lengo la kukutana huko lilikuwa ni kumtambulisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Bw. Emmanuel Lameck Mkilia kwa wizara hiyo pamoja na kuanzishwa ofisi za Tume hiyo Zanzibar.

Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi imeanzishwa mwaka huu mara baada ya kupitishwa kwa  Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Na. 11 iliyotungwa na Bunge mwaka jana 2022 na kuanza kutumika Mei, 2023 mara baada ya kusainiwa na Rais wa Jamhuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.