Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

NAIBU WAZIRI MAHUNDI AHITIMISHA ZIARA YA SIKU 3 KUTEMBELEA TAASISI NA WATOA HUDUMA ZA MAWASILIANO MKOANI DAR ES SALAAM


Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amehitimisha ziara yake ya siku tatu ya kutembelea taasisi na watoa huduma za mawasiliano zilizopo Mkoa wa Dar es Salaam.

Amehitimisha ziara yake tarehe 12 Septemba, 2024 kwa kutembelea Kampuni ya TIGO ambapo amefurahishwa na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Kampuni hiyo sanjari na kutoa ajira kwa zaidi ya vijana mia tano (500).

Amesema uwekezaji uliofanywa unaendana na kasi ya dunia zaidi wakiungana na Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kuhakikisha huduma za Mawasiliano zinatolewa kwa ufanisi mkubwa.

Ziara yake Jijini Dar es Salaam imehusisha Kampuni ya Airtel, Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na kuhitimisha Kampuni ya TIGO.