Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

MIUNDOMBINU BORA KIJIJI CHA  MSOMERO


Na Chedaiwe Msuya, WHMTH 


Serikali kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeshiriki kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara za kisekta na kutembelea kijiji cha Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga kujionea hatua mbalimbali za ujenzi wa miundombinu kabla ya kuanza kwa awamu ya pili ya kuhamisha wananchi wanaoishi katika hifadhi ya Ngorongoro waliojiandikisha kuhama kwa hiari.

Serikali inaendelea na zoezi la kuandikisha wananchi wanaohama kwa hiari katika hifadhi ya Ngorongoro na kuwapeleka katika maeneo mengine ili kulinda hifadhi na kuimarisha maisha ya wananchi nje ya eneo hilo.

Aidha, Serikali imejipanga katika kuhakikisha kuwa wizara zote za kisekta zinashiriki kikamilifu katika kuhakikisha kuwa miradi iliyopo katika Kijiji Cha Msomera inakamilika kwa wakati ili kuwezesha wananchi wanaoendelea kujiandikisha kuhamia katika eneo hilo.

Nae, Mkuu wa Wilaya ya Halmashauri ya Handeni Mhe. Albert Msando amepongeza makatibu wakuu kwa uwepo wao katika ziara hiyo na kutoa shukrani kwa Jeshi la polisi kuendelea na kazi licha ya hadha kubwa ya mvua Msomera. 

Martin oleikayo Mwenyekiti wa Kijiji Cha Msomera amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa upendo alionao katika kuhakikisha Kijiji Cha Msomera kinaendelea kuwa na Miundombinu Bora ikiwemo Barabara, Maji na Umeme. 

Katika ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu wa WHMTH, Bw. Selestine Gervas Kakele aliambatana na Mkurugenzi Huduma za Mawasiliano, Bw. Mulembwa Denis Munaku pamoja na watumishi wengine wa Wizarani. 

UJenzi wa Msomera unaekela katika awamu ya pili ambapo takribani ya nyumba 5,000 na kati hizo nyumba 2500 zipo katika hatua nzuri ya ujenzi