Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

MHANDISI MAHUNDI ASHIRIKI MKUTANO WA 27 WA MAENDELEO YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA USWISI


Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Maryprisca amehudhuria Mkutano wa 27 wa Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia Duniani ulioandaliwa na United Nations Conference on Trade and Development (UNCTAD) na kufanyika nchini Uswisi.  

 Katika mwaliko huo Mhe. Mhandisi Maryprisca aliambatana na Balozi wa Kudumu wa Tanzania nchini Uswisi Mhe. Dkt Abdallah Possi na Mkurugenzi Msaidizi wa Uendelezaji wa Mifumo na Huduma za TEHAMA Mhandisi Peter Mwasalyanda.

Katika kikao hicho mambo mbalimbali yalijadiliwa ikiwa ni pamoja na namna ambavyo Tanzania inaweza kunufaika na fursa mbalimbali zilizopo ITU hasa katika masuala ya Miundombinu ya TEHAMA, Mafunzo kwa Wataalam wa TEHAMA nchini na masuala ya Usalama Mtandao, na Teknolojia zinazoibukia (Emerging Technologies).