Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

MAFUNZO YA KUJENGA UWEZO KUHUSU MFUMO WA ANWANI ZA MAKAZI KATIKA HALMASHAURI YA MJI MAFINGA YAFANYIKA MAFINGA


Na. Simon Kibarabara, IRINGA

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kupitia wataalamu wake wa NaPA imeendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi, watendaji na wataalamu wa Halmashauri ya Mafinga Mjini kuhusu mfumo wa Anwani za makazi.

Mafunzo hayo yamefunguliwa na Mkuu wa Wilaya Mhe. Dkt. Linda Kasekwa Leo tarehe 21, Novemba, 2023 katika ukumbi wa Halimashauri hiyo. 

Mhe. Dkt. Kasekwa ameeleza kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha Kila mwananchi anatambulika na kufikiwa Kwa kutumia anwani ya makazi, hatua ambayo itawezesha kuimarisha maisha ya wananchi na kuweka mazingira ya kunufaika na fursa mbalimbali za kijamii na kiuchumi hususani uchumi wa kidijitali.
 
Aidha, Mhe. Kasekwa aliwasisitiza viongozi kuwa mafunzo hayo ni nyenzo muhimu katika kutekeleza majukumu yao na kusimamia zoezi zima la Anwani za Makazi katika maeneo yao.

"Kila Mtendaji kata na Mitaa aandae Mpango kazi wa kuhakikisha Wananchi wote katika eneo lake wanakuwa na Anwani za Makazi” Mhe. Kasekwa amesisitiza. Aidha amemwelekeza Mkurungenzi wa Mji wa Mafinga aangalie uwezekano wa kuwezesha utekelezaji wa shughuli za Anwani za Makazi ndani ya Mji wa Mafinga Mjini.
   
Kwa Upande wake  Mhandisi. Jampyon Mbugi, Mratibu wa Anwani za Makazi kitaifa 
 ametumia nafasi hiyo kuwataka Wenyeviti na Watendaji wa Mitaa kushirikiana na wajumbe wa Serikali za Mitaa pamoja na wananchi kwa ujumla ili kuhakikisha kazi ya kuhakiki taarifa za Anwani za Makazi inafanikiwa na kuleta tija iliyokusudiwa. 

Aidha Mhandisi. Mbugi  ameeleza kuwa Zoezi hilo niendelevu Kwa lengo la kuwajengea uelewa Watanzania juu ya matumizi na umuhimu wa Anwani za makazi hapa nchini. 

Pia  amewakumbusha wananchi kuwa Anwani za Makazi ni rasilimali inayosukuma maendeleo kwa haraka na wakati unaostahili, hivyo katika  usimamizi wa zoezi hili wadau wanapaswa kuwa makini katika kuhakiki taarifa zote kwenye maeneo husika.