Habari
KATIBU MKUU WHMTH AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA MAENDELEO YA UJUZI, UJASIRIAMALI NA TEHAMA, INDIA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Mohammed Khamis Abdulla amekutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Rajeev Chandrasekhar, Waziri wa Maendeleo ya ujuzi, ujasiriamali na TEHAMA wa Serikali ya India ambapo wamejadili namna India na Tanzania wanaweza kufanya mashirikiano katika sekta ya TEHAMA.
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na katibu Mkuu huyo upo katika mji wa Pune, India kushiriki mkutano wa 3 wa kikundi cha kidijitali cha mataifa 20( G2O).