Habari
KATIBU MKUU ABDULLA AONGOZA WATUMISHI KUPANDA MITI
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Mohamed Khamis Abdulla leo tarehe 31 Januari, 2024 ameongoza watumishi wa wizara katika zoezi la upandaji miti mbele ya Jengo la Ofisi Mpya za Wizara zilizopo Mji wa Serikali - Mtumba, Dodoma.
Zoezi hilo limehudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Selestine Gervas Kakele na kushuhudiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Bw. Abdallah Mitawi.
Tukio hilo la Upandaji Miti ni sehemu ya shamrashamra kuelekea sherehe za maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.