Habari
KATIBU MKUU ABDULLA AKUTANA NA UJUMBE WA UBALOZI WA MAREKANI NCHINI

Na Chedaiwe Msuya, WHMTH, Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Mohammed Khamis Abdulla amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka ubalozi wa Marekani nchini ambao ni Mshauri wa Kisiasa na Uchumi Bwn, Jonathan Howard pamoja na Mkuu wa Siasa Bw, Richard Allen ambapo wamezungumzia masuala mbalimbali kuhusu Teknolojia ya 5G, masuala ya Usalama wa Mtandao pamoja na Uhuru wa vyombo vya habari nchini.
Aidha, wameipongeza Serikali kupitia Wizara hiyo kwa kukuza uhuru wa vyombo vya habari nchini na kuboresha Sheria inayosimamia huduma za habari nchini.
Kikao hicho kiliudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mha. Stephen Mwita Wangwe kimefanyika leo Septemba 7, 2023 katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma