Habari
DKT YONAZI ATEMBELEA KIWANDA CHA SMART CARD CHA DZ CARD AFRICA LTD
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi Septemba 09, ametembelea kanda maalum ya Kiuchumi ya Benjamin William Mkapa Mabibo Jijini Dar es Salaam.
Dkt. Yonazi amekagua na kujionea kazi mbalimbali zinazofanywa na kiwanda cha kutengeneza SMART CARD cha DZ CARD AFRICA LIMITED kama anavyoonekana katika picha mbalimbali akiwa na maafisa wa Wizara hiyo alioongozana nao, Uongozi wa EPZA na kiwanda cha DZ CARD AFRICA LIMITED.
Akizungumza mara baada ya kukagua kazi za kiwanda hicho Dkt. Jim Yonazi ameahidi kutoa ushirikiano Zaidi katika kukuza Teknolojia na Uwekezaji nchini kwa ujumla ili kuendeleza dhamira njema ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kukuza uchumi wa Nchi na kuongeza ajira kwa Watanzania.