Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

CHUO KIKUU TANZANIA CHABUNI SATELITE YAKE, WHMTH YAPONGEZA HATUA HIYO


Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Kundo Mathew (Mb) amekipongeza Chuo Kikuu cha Mt. Joseph kwa hatua nzuri waliyofikia ya kuwa wakwanza nchini kuunda Satelite yao.

Naibu Waziri Kundo ameyasema hayo wakati wa Hafla ya Uzinduzi wa Maonesho ya Chuo Kikuu cha Mt. Joseph Nchini Tanzania (TAN-TECH2023), viwanja vya Mlimani City, Dar es Salaam, Tarehe 06 Julai, 2023.

“Moja kati ya bunifu kubwa ambazo nimeona zinazofanyika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph Nchini Tanzania ni katika teknolojia ya satelaiti (Satellite Technology), ambao nimeambiwa unatekelezwa na timu ya wahadhiri na wanafunzi wetu wa idara mbalimbali kwenye Ndaki ya Uhandisi na Technolojia. Wizara inaahidi kwamba itasaidia ili kufanikisha utafiti huu, hasa katika kuwezesha ushirikiano na taasisi nyingine na kupata huduma za kurusha satellite.” amesema mhandisi kundo

“Nikiwa Naibu Waziri kwenye Wizara inayoshughulikia masuala ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari nimepata imani kubwa na ujasiri wa kusema kwamba hakika kupitia vijana wetu tutaifikia malengo yetu ya kurusha satellite kwa muda mfupi kuliko tunavyodhani. Tukijipanga vizuri na kuwatumia hawa wanataaluma na vijana wetu ipasavyo Tanzania inaweza kupeleka satellite angani muda mfupi ujao.” amesema mhandisi Kundo.

Pia Naibu Waziri Kundo alisema kuwa Maonesho hayo yamedhihirisha kwamba elimu inayotolewa Tanzania, hususan Chuo Kikuu cha Mt. Joseph Nchini Tanzania, ni ya kiwango cha juu na wahitimu wetu hawana tofauti na wahitimu wa nchi nyingine duniani.